Misemo na methali za Kiingereza 1
(English sayings and proverbs 1)
Too many cooks spoil the broth.
Photo by Gaelle Marcel via Unsplash
(Wapishi wengi mno huharibu mchuzi.)
Msemo huu kwa Kiingereza unamaanisha kuwa jambo au mradi wowote ule huharibika ikiwa utasimamiwa na watu wengi kwa wakati mmoja.
too (mno) many (ingi)
cook (mpishi) spoil (haribu)
broth (mchuzi)
Ni sawa na kusema: Mikono mingi harabu ya upishi.
Do not count your chickens until they hatch.
Photo by Daniel Tuttle via Unsplash
(Usihesabu kuku wako kabla hawajatotolewa.)
Usifanye mipango kwa kutegemea kuwa jambo fulani zuri litatokea kabla hujawa na uhakika kuwa limeshatokea kwa hakika, hasa hasa kuhusu pesa! (Sio kila yai hutotowa kifaranga!)
count (hesabu) chicken (kuku)
until (mpaka) hatch (totowa)
You could have knocked me down with a feather (when it happened).
Photo by Ibrahim Rifath via Unsplash
(Ungeweza kunishinda kwa unyoya tu (ilipotokea).)
Nilishtushwa sana (kiasi kwamba kitu chochote kidogo kingeweza kunifanya nianguke)!
could have –(ingeweza (ingaliweza) ) knock down – (angusha chini) feather – (unyoya)
I wished the ground had opened up and swallowed me.
Photo by Ronan Furuta via Unsplash
(Nilitamani ardhi ipasuke inimeze.)
Nilifadhaishwa sana kiasi nilitamani nipate pahala pa kujificha.
wish (tamani) the ground (ardhi)
open up (funguka) swallow (meza)
Follow us for more articles like this.
Tufuate kwenye kwa maudhui kama haya zaidi.
If you like this content, share it on Twitter or Facebook.
Kama unapenda maudhui haya ishiriki kwenye Facebook, Twitter.
0 Comments