Viwango vya Kiingereza

Wakati wa kuchagua nyenzo za kufundisha au kusoma, inasaidia kuelewa viwango tofauti ambavyo wanafunzi wa Kiingereza wameainishwa, na wewe au wanafunzi wako mpo katika kiwango gani.

Viwango hivi vimeonyeshwa hapa chini. Piramidi hutumiwa mara nyingi kwa sababu kuna watu wengi zaidi wanaosoma katika viwango vya chini vya Kiingereza kuliko vile vya juu.

Piramidi hii inaonyesha viwango vya kisasa (CEFR) (A1 – C2), na viwango sawa vya jadi/kitambo vimeonyeshwa upande wa kulia:

CEFR inasimamia Common European Framework of Reference (Mfumo wa Marejeleo wa Kawaida wa Ulaya) kwa ajili ya lugha, mfumo ambao umeundwa katika Ulaya ili kutumika kwa idadi kubwa ya lugha, ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kihispania na Kijerumani.

Kumbuka: Beginner (level) imeongezwa na watayarishaji wengi wa vitabu vya kiada katika miaka ya hivi karibuni. Imeundwa kwa ajili ya wanafunzi ambao wanaweza kuhitaji maandalizi kabla ya kusoma Elementary (level). Sababu za hii zinaweza kujumuisha (i) kutofahamu kabisa Kiingereza, (ii) kuzungumza lugha tofauti sana na Kiingereza na/au kutumia alfabeti tofauti na (iii) kuwa na ugumu wa kuendana na kasi ya kozi Elementary.

Advanced (2) ni kiwango ambacho kwa ujumla husomwa na wataalamu wa lugha kama vile watafsiri na walimu wa lugha. Ni kiwango ambacho wazungumzaji wengi wa kiasili hawajafikia.

Makala hii ina viungo vya kufanya majaribio ya mtandaoni bila malipo ambapo unaweza kujua kiwango chako cha Kiingereza.

(Kiingereza.com inaangazia zaidi Kiingereza cha Uingereza. Ikiwa unahitaji kujua viwango sawa vya Kiamerika (Marekani hutumia kipimo tofauti), makala hii (kwa Kiingereza) ni muhimu.)

English Levels

When choosing materials for teaching or study, it helps to understand the different levels English learners are categorised into, and which level you or your students are at.

These levels are shown below.  A pyramid is often used because there are many more people studying at the lower levels of English than the higher ones.

The pyramid shows the modern (CEFR) levels (A1 – C2), with the equivalent traditional levels shown on the right:

CEFR stands for the Common European Framework of Reference for languages, a system that has been designed in Europe to be applied to a large number of languages, including English, French, Spanish and German.

Note:  Beginner level has been added by many textbook producers in recent years.  It is designed for students who may need some preparation before studying Elementary level.  Reasons for this may include  (i) Being completely unfamiliar with English, (ii)  speaking a language very different to English and/or using a different alphabet and (iii) having difficulty keeping up with the speed of an Elementary course.

Advanced (2) is a level only generally studied by language professionals such as translators and language teachers.  It is a level many native speakers have not attained.

This article contains links to free online tests where you can find out your level of English.

(Kiingereza.com focuses mostly on British English.  If you need to find out the equivalent American levels  (the US uses a different scale), this article is useful.)

Misemo na methali za Kiingereza 2 (English sayings and proverbs 2)

A bad workman always blames his tools.(Mfanyakazi (fundi) mbaya, hulaumu zana zake.) Msemo huu husemwa ambapo mtu hulaumu kosa au kufeli kwa kuhusisha na zana anazotumia kufanyia kazi. (Mara nyingi huwa ni yule mtu anayetumia zana na namna gani anazitumia na hilo ndio...

Kiingereza Bora Zaidi barani Afrika

Nchi hizi za Kiafrika zinazungumza Kiingereza bora zaidi, kulingana na EF Education First, kampuni ya elimu inayojishughulisha na ufundishaji wa lugha. Tanzania iko nafasi ipi na utafiti wa EF ni sahihi kiasi gani? Kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa EF, nchi...

Misemo na methali za Kiingereza 1 (English sayings and proverbs 1)

Misemo na methali za Kiingereza 1 (English sayings and proverbs 1)Too many cooks spoil the broth.Photo by Gaelle Marcel via Unsplash(Wapishi wengi mno huharibu mchuzi.)Msemo huu kwa Kiingereza unamaanisha kuwa jambo au mradi wowote ule huharibika ikiwa utasimamiwa na...

Kamusi za Mtandaoni za Wanafunzi wa Kiingereza (na zingine ambazo zinaweza kutumika nje ya mtandao)

Kuna idadi ya kamusi zinazopatikana bila malipo mtandaoni ambazo zinaweza kusaidia katika kusoma Kiingereza. Baadhi yazo pia zinaweza kupakuliwa kama programu na kutumika nje ya mtandao. Hapa kuna baadhi ya zile bora, kwa wakati wa kuandika:Kamusi za Lugha mbili...

Viungo kwa wazazi na watoto

Wasaidie watoto wako kujifunza Kiingereza Kuna idadi ya nyenzo kwenye mtandao ambazo unaweza kutumia na watoto wako kuboresha Kiingereza chao, ambacho nyingi ni bure. Ifuatayo ni uteuzi wa nyenzo zile  bora zaidi:VIFAA BILA MALIPO KUTOKA UINGEREZABritish...

Oxford na Cambridge ni nini?

Katika kujifunza Kiingereza, kuna uwezekano utakutana na majina haya. Oxford na Cambridge ni majina ya miji nchini Uingereza ambapo vyuo vikuu viwili vya zamani zaidi, vya kifahari zaidi, Chuo Kikuu cha Oxford na Chuo Kikuu cha Cambridge, viko.                     ...

Majaraibio (ya Bila Malipo) ya Kiingereza Mtandaoni

Jua kiwango chako ili uweze kupata nyenzo za kujifunzia zinazokufaa Ni muhimu kujua kiwango chako cha Kiingereza ili kujua ni nini unapaswa kusoma ili ujiboreshe. Kuna idadi ya majaribio ya bila malipo yanayopatikana mtandaoni ili kukusaidia kujua kiwango chako.BBC...

Sababu 5 kwa nini hujajifunza Kiingereza

Watu wengi wanaona aibu kwa sababu hawawezi kuzungumza Kiingereza kama marafiki na wafanyikazi wenzao. Hata hivyo, unapaswa kufahamu kwamba kuna sababu kadhaa za hukujifunza lugha ya Kiingereza hapo awali, ambazo huenda zisiwe kosa lako:1 Hakuna aliyezungumza nawe kwa...
0 Comments
Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us for more articles like this.
Tufuate kwenye kwa maudhui kama haya zaidi.

If you like this content, share it on Twitter or Facebook.
Kama unapenda maudhui haya ishiriki kwenye Facebook, Twitter.